FURSA YA MAFUNZO YA BURE KUKUZA UJUZI KWA NJIA YA UANAGENZI

 1. 1.      Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi kwa njia mbali mbali ikiwemo uanagenzi, mafunzo ya vitendo mahali pa kazi na utambuzi wa ujuzi uliyopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo. Katika kufanikisha utekelezaji wa Programu hii, Ofisi ya Waziri Mkuu imeingia mkataba na Taasisi ya  Don Bosco Net Tanzania  iliyopo Oysterbay Dar es salaam wa kutoa mafunzo katika fani mbalimbali. Lengo ni kuwezesha vijana kuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na kuongeza wigo mpana wa kujiajiri au kuajiriwa au kuendelea na mafunzo ngazi ya juu. Fani zitakazofundishwa ni Kubuni Mitindo ya Mavazi na Ushonaji, Ufundi Bomba, Useremala, Uchomeleaji Vyuma, Uchongaji wa Vipuri vya Mitambo, Uashi, Uwekaji waTerrazo na Vigae kwenye majengo, Ufundi Magari na Mitambo, Kilimo na Ufugaji, Kutengeza Komputa, Kuchapa Vitabu na Nyaraka, pamoja na Kufunga Umeme ukiwemo wa mwanga wa jua (Solar) wa majumbani na viwandani. Mafunzo ya kukuza ujuzi yanafanyika Mikoa yote ya Tanzania Bara na yataanza kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itaanza Mwezi Julai inayojumuisha mikoa 12 na Awamu ya pili itaanza Mwezi Agosti, 2019 itakayojumuisha mikoa 14.

   

   

   

  2.      Mikoa na Vituo vitakavyotoa Mafunzo

  Vituo vilivyokubalika na Serikali kutoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania pamoja na fani zitakazotolewa ni:

   

   

  ENEO

  CHUO

  FANI

  1

  MUSOMA - MARA

  ST. ANTHONY VTC

  Ufundi umeme

  Kubuni mitindo ya mavazi na Ushonaji

  Uashi

  Mapishi ya vyakula

  2

  GEITA (Location: Moringe sokoine & Sophia Town)

  GEITA VOCATIONAL TRAINING CENTER

  Ufundi magari

  Ufundi umeme

  Ufundi umeme wa magari

  Kubuni mitindo ya mavazi na ushonaji

  Utengenezaji wa kompyuta

  Uashi

  Ufundi bomba

  Useremala

  Kuweka terrazzo na vigae

  3

  DAR ES SALAAM

  DON BOSCO OYSTERBAY VTC

  Ufundi wa magari

  Useremala

  Uchomeleaji vyuma

  Uchongaji vipuri

  Terrazo na Vigae

  Kutengeneza Kompyuta

  Ufundi umeme

  Ufundi umeme wa jua (solar)

  Kubuni mitindo ya mavazi na ushonaji

  MATUMAINI YOUTH TRAINING CENTRE

  Mapishi ya vyakula

  Utengenezaji wa kompyuta

  Kubuni Mitindo ya Mavazi na Ushonaji

  DON BOSCO YOUTH CENTRE UPANGA

  Kutengeneza Kompyuta

  Kubuni mitindo ya Mavazi na Ushonaji

  4

   

  DODOMA

  DON BOSCO DODOMA TECHNICAL INSTITUTE

  Ufundi magari

  Useremala

  Ufundi Bomba

  Uashi

  Terrazo na Vigae

  Mapishi ya vyakula

  Kutengeneza kompyuta

  Kuhudumia vyakula na vinywaji

  Uchomeleaji vyuma

  Uchongaji vipuri

  Ufundi umeme

  Ufundi umeme wa jua (solar)

  Kubuni Mitindo ya mavazi  na Ushonaji

  5

  IRINGA

  DON BOSCO YOUTH TRAINING CENTRE IRINGA

  Ufundi magari

  Useremala

  Ufundi Bomba

  Uashi

  Utengenezaji Kompyuta

  Uchomeleaji Vyuma

  Ufundi Umeme

  Ufundi umeme wa Jua

  Kubuni Mitindo ya mavazi na ushonaji

  DON BOSCO MAFINGA

  Utengenezaji wa Kompyuta

  Kubuni Mitindo ya Mavazi na Ushonaji

  6

  SHINYANGA

  OLA SISTERS VTC-BUGISU

  Kutengeneza Kompyuta

  Ufundi Umeme

  Uchakataji wa vyakula ( food processing)

  Kubuni mitindo  ya mavazi na ushonaji

  ST. FRANCIS DE SALES TECHNICAL INSTITUTE- MWAKATA- ISAKA

  Kubuni Mitindo ya Mavazi na Ushonaji

  7

  ARUSHA

  KIITEC-MOSHONO

  Ufundi Umeme wa Jua (solar)

  Kutengeneza Kompyuta

  Ufundi umeme

  8

  MOSHI - KILIMANJARO

  DON BOSCO MOSHI

  Kutenegeneza Kompyuta

  Mafunzo ya ufugaji

  Kilimo cha matunda, maua  (horticulture crops)

  9

  BUKOBA - KAGERA

  KASHOZI HOME CRAFT VTC

  Kubuni mitindo ya mavazi  na Ushonaji

  Mapishi ya vyakula

  10

  SINGIDA

  RC MISSION VTC MANYONI

  Kubuni mitindo ya  mavazi na ushonaji

  Mapishi ya vyakula

  11

  LINDI

  LINDI RVTSC - VETA

  Uchomeleaji Vyuma

  Ufundi umeme

  useremala

  Uashi

  Ufundi magari

  12

  RUVUMA

  PERAMIO VOCATIONAL TRAINING CENTRE

  Kubuni Mitindo ya Mavazi na Ushonaji

  Ufundi magari

  Ufundi bomba

  Ufundi umeme

  Kuchapa vitabu, Makala na nyaraka

  Uashi

  Ufugaji

  Useremala

  Utengenezaji wa Komyuta

  13

  MOROGORO

  HOLY CROSS SOCIAL TRAINING CENTRE

  Kubuni mitindo ya mavazi na ushonaji

  Utenegenezaji wa kompyuta

   Mapishi ya Vyakula

   

  3.      Sifa za Kujiunga na Mafunzo

  Kwa wote wanaopenda kujiunga na mafunzo wanapaswa kuwa na sifa zilizoainishwa hapa chini :

  (a)           Elimu ya Msingi au zaidi kwa fani za Nguo, Mitindo na Ushonaji, Ufundi bomba, Ujenzi, Useremala, Uchomeleaji na Uungaji vyuma;

  (b)          Elimu ya kidato cha nne kwa fani ya Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi magari, umeme wa majumbani na viwandani, TEHAMA, Umeme wa magari, Umeme wa jua (Solar) na kuchapa vitabu;

  (c)          Awe Mtanzania;

  (d)          Awe na umri kati ya miaka 18 – 35; na

  (e)          Awe mwenye Afya njema

   

  4.      Fomu zitatolewa  bila malipo katika vyuo husika kuanzia tarehe  tarehe 17  hadi 23 Julai, 2019.  Mwombaji anatakiwa kurudisha fomu kuanzia tarehe 24-26 Julai ikiambatana na:

  (a)          Barua ya maombi yenye anuani kamili ikiwa na namba za simu pamoja na barua pepe (kama anayo);

  (b)          Nakala ya Cheti cha Elimu uliyohitimu;

  (c)          Nakala ya Cheti cha kuzaliwa au Kitambulisho cha uraia au kadi ya mpiga kura;

  (d)          Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa anaoishi mwombaji (lazima); na

  (e)          Picha nne za paspoti zenye rangi ya bluu kwa nyuma.

   

  5.      Vijana  watakao kidhi vigezo watafadhiliwa na Serikali kwa asilimia 100 kwa kulipiwa ada ya mafunzo yatakayofanyika katika vyuo vilivyotajwa hapo juu kwa muda wa miezi sita. Kijana atakayechaguliwa atagharamiwa  kiasi cha Tsh. 100,000/- kwa mwezi kama nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani. Majina ya vijana wote waliochaguliwa kushiriki mafunzo yatatolewa magazetini na tovuti za vyuo husika kuanzia tarehe 1 Agosti mpaka tarehe 5 Agosti. Mafunzo ni ya kutwa na yataanza rasmi tarehe 19 Agosti, 2019. Hivyo, inashauriwa kwamba kijana kuomba mafunzo haya katika kituo kilicho karibu au ambapo atapata pa kuishi. Mwombaji atatakiwa kurejesha fomu ya maombi yeye mwenye katika chuo husika kabla ya tarehe 26 Julai, 2019. Tangazo la mafunzo katika mikoa mingine ya awamu ya pili litatolewa kuanzia tarehe 22 Julai, 2019.

  Imetolewa na :

   

  Katibu Mkuu,

  17.07.2019

TOP